Rashid Msiri
Mwanakwetu Sports
Kila filimbi inapolia ni mwanzo mpya wa hisia kali zisizo mithirika kwa mashabiki wa mchezo soka na kila mguso mmoja wa mpira hutafsiri mamia ya ndoto, matamanio ya mashabiki na wachezaji wa wapo kiwanjani.
Mpira wa miguu umeendelea kuwa mchezo unaoingunisha dunia moja kwa moja kupitia michuano mbalimbali iliyopo ulimwenguni kote, kwani mchezo wa kabumbu ni zaidii ya dakika 90, ni zaidii ya maisha kwa vizazi na vizazi.
Mjukuu wangu kalamu hii nimeishika si kukuhadithi hadithi zisizo kwisha za abunuasi ama vihoja vya bawabu mlinzi wa mlangoni, hapana ila kalamu hii imekuja kukurithisha historia iliyoshiba juu ya michuano ya mataifa barani Afrika (African Cup of Nation) Afcon.
Mnamo mwaka 1957 ndio kwa mara ya kwanza ardhi ya Afrika iliyoshuhudia kuanza kwa safari ndefu iliyojaa vihoja vyenye ufundi na Radha kamili ya vipaji vya soka kutokea barani Afrika, ikiwa kwa kipindi hicho nchi nyingi bado zilikuwa chini ya mkoloni.
Licha ya hayo yote haikuziia ngami kupita kwenye tundu la sindano ama nahodha kutia nanga kwenye pwani ya Tsunami, watu wa chache wabeba maono wakiongozwa na raisi wa shirikisho la soka barani Afrika CAF (confederation of African football) bwana Abdelaziz Abdallah Salem kutokea nchini Misri.
Kutokana na mataifa mengi kwa kipindi hicho kuwa bado yapo kwenye uangalizi wa wakoloni michuano hiyo ilishuhudia ushiriki wa mataifa machache sana kwani Ni timu 3 tu ziliweza kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza ambayo ilifanyika NCHI Sudan.
TIMU ZIPI ZILISHIRIKI AFCON KWA MARA YA KWANZA?
Huko nchini Sudan ikiwa ni moja ya maeneo yaliyokuwa yamepiga hatu kubwa kwa miaka hiyo ndipo michuo ya Afcon ilifanyika kwa mara ya kwanza huku ikikutanisha timu 3 pekee ambazo ni Egypt, Sudan na Ethiopia.
Lakini hapo awali michuano hiyo ilitarajiwa kukutanisha timu nne lakini taifa la nne lililotarajiwa kushiriki katika michuano hiyo halikuweza kufika kwenye michuano hiyo ambalo lilikuwa ni taifa la Gabon kutokana na kuwa kipindi hicho bado lilikuwa linatawaliwa hivyo basi maamuzi ya mtawala ndiyo yalisababisha wao kushindwa kwenda nchini Sudan kwa wakati huo.
Mchezaji Ad-Diba kutokea nchini Egypt ndiye mchezaji wa Kwanza kwenye historia ya michuano ya mataifa barani Afrika kufunga bao la kwanza kwenye michuano hiyo katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya wenyeji Sudan.
Michuano hiyo kwa mara ya kwanza ilishuhudia taifa la Misri likitangazwa kuwa ndio mabingwa kwa mara ya Kwanza wa michuano ya mataifa barani Afrika huku waki kabidhiwa taji la michuano hiyo ambapo kikombe hicho kilipewa jina la raisi wa kwanza wa CAF bwana Abdelaziz Abdallah Salem kutokea nchini Misri.
KUBADILIKA KWA MUUNDO WA KOMBE HILO KWA NYAKATI TOFAUTI.
Hadi hivi Sasa Afrika imekwisha kushuhudia zaidii ya vikombe vitatu vikibadilika kwa nyakati tofauti tofauti kutokana na sababu mbalimbali.
Kombe la kwanza lililopewa jina la raisi wa kwanza wa CAF bwana Abdelaziz Abdallah Salem baada ya taifa la Misri kubeba Kikombe hicho mara 3(1957,1959 na 1978) kwa hiyo kutokana na taratibu za shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa kipindi hicho iliwabidi kuwapa taifa la Misri kombe hilo na wao kubuni kikombe kipya.
Mnamo 1980 huko nchini Nigeria kitambulisho kikombe kipya kama taji kwa bingwa wa michuano ya mataifa barani Afrika ambacho kilijulikana kama Unity Cup kwani lengo kubwa lilikuwa ni kuonyesha umoja wa Afrika.
Lakini taji hilo halikudumu vile vile kutokana na taifa la Ghana kubeba kombe hilo mara 3 Kwa nyakati tofauti ikiwa ni 1984,1988 na 2000.
Muonekano wa Sasa wa kombe la mataifa barani Afrika ndiyo muonekano wa 3 ambao umepewa jina la CAF trophy ikiwa lilianza kutumika rasmi kwenye Afcon ya mwaka 2001 huko nchini Mali, lakini licha ya taifa Misri kuwahi kulitwa taji hilo mara 3 mtawaliwa hakuweza kukabidhiwa kombe hilo ila Kwa sheria za sasa bingwa hupewa mfano wa tajiri hilo kama ilivyokuwa kwenye michuano ya kombe la Dunia.
JE UNAMFAHAMU BINGWA WA MUDA WOTE WA MICHUANO YA AFCON?
Hadi hivi Sasa Taifa la Misri linashikilia rekodi ya kuwa ndio taifa lililotwa taji la michuano ya mataifa barani Afrika mara nyingi zaidii kwani imetwa taji hilo kwa makala 7 tofauti ya michuano hiyo.
Mataifa mengi yaliyotwa taji hilo ni Cameroon 5, Ghana 4, Nigeria 3, Ivory coast 3.
NI NANI MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE WA MICHUANO YA AFCON?
Samweli Etoo ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye michuano ya mataifa barani Afrika akiwa ameingia kambini mara 18 katika makala 6 za michuano ya Afcon aliyoshiliki huku akitwa taji hilo mara mbili mtawaliwa 2000,2002 akiwa na taifa la Cameroon.
HUYU NDIYE MUAMUZI MWENYE FAINALI ZA AFCON NYINGI HADI SASA.
Mchezo wa soka haukamiliki hadi pale sheria 17 za mchezo huo zinapokuwa zimetimizwa na hapa ndipo jina la Tesfaye Gebreyesus kutokea nchini Ethiopia linatajwa na wahenga wa mchezo wa soka barani Afrika kuwa ndio kielelezo cha ubora wa watao hukumu ndani ya dakika 90 kutokea barani Afrika kwani makala na majarida mbalimbali yamemuonyesha kuwa ndiye mtu pekee aliyechezesha mechi nyingi za fainali za michuano hiyo.
Tesfaye Gebreyesus ameshezesha fainali 6 za michuano ya afcon ikiwa ni 1970,1974,1978,1980,1984 na 1986.
Hii inaonesha alikuwa muamuzi mwenye uwezo wa hali ya juu katika kutafsri sheria za soka kwa wakati huo.
WACHEZAJI WALIOSHIRIKI MICHUANO MINGI YA AFCON.
Nyota kutokea nchini Cameroon RigoBert Song ameshiriki makala 8 za michuano ya Afcon tangu 1996-2010,
mwingine ni nyota kutokea Taifa la Misri nyota Ahmed Hassan yeye ameshiriki makala 8 za michuano ya afcon ila anashikiria rekodi ya kucheza fainali nne za michuano hiyo 1998,2006,2008 na 2010.
Nyota Andre Aye wa Ghana na Yousse Msakini wa Tunisia na wanashikiria rekodi ya kucheza makala 8 za michuano ya afcon kwa nyakati tofauti.
KOCHA ALIYECHEZA MICHUANO MINGI YA AFCON.
Jina la Claude De Roy ni moja kati ya makocha waliweza kuingia kwenye rekodi ya shirikisho la soka barani Afrika CAF ya kuwa ndiye kocha aliyeshiriki makala nyingi za Afcon akiwa na michuano 9 ya Afcon kwa mataifa tofauti kuanzia mwaka 1986-2017.
Mataifa ambayo Claude De Roy ameweza kufundisha kwa bara la Afrika ni Cameroon 1986-1988, Senegal 1990-1992, Ghana 2008, Dr congo 2006,2013, Congo 2015 na Togo 2017 hii inamfanya De Roy kuwa mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa zaidii wa michuano ya afcon.
Licha ya rekodi zote za kushiriki Afcon mara nyingi lakini bado Claude De Roy sio Kocha mwenye mataji mengi ya kombe la Afcon bali rekodi hiyo inashikiliwa na Charles Gamfyi kutokea Ghana aliyechukua taji hilo mara 3 ikiwa ni 1963,1965 na 1982 huku akifunga na Kocha wa taifa la Misri Hassan Shehata mwenye rekodi ya kipekee kuchukua taji hilo mara 3 mfululizo ikiwa ni 2006,2008 na 2010.
Licha ya yote hayo kocha Hervé Renard ndiye kocha mwenye rekodi ya kuchukua Taji la Afcon akiwa na mataifa mawili tofauti ikiwa ni Zambia 12 na Ivory coast 2015.
REKODI ZA KUSTABIJISHA AFCON HADI SASA.
Mechi ya zaire ambayo ni DR CONGO kwa sasa dhidi ya Sudan ndiyo mchezo unaoshikikilia rekodi ya kuhusisha mabao mengi kufungwa kwenye mchezo mmoja ambapo mchezo huo ilishuhudia Sudan ikibugizwa bao 9-0 ambapo Hadi hivi Sasa ndio kimerekodiwa kama kipigo kikubwa zaidii katika michuano ya Afcon.
Ikiwa haya ni makala ya 35 michuano ya Afcon ni kilele cha juu zaidi ya uadilifu na ustaarabu wa mchezo wa mpira wa soka kwa vizazi na vizazi hivyo kizazi cha Sasa cha teknolojia kinacho cha kujivunia kwa ushiriki wao Katika michuano hiyo.
rashidmsiri@gmail.com
0754645826







Post a Comment