Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ameweka wazi hisia zake baada ya kukiri kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikuwa tayari kumruhusu kuondoka, kabla ya yeye mwenyewe kuamua kubaki Old Trafford.
Akizungumza na Moja ya chombo Cha habari , Fernandes alisema alipata hisia kuwa upande wa klabu usingepata shida endapo angeondoka, akisema uamuzi wa kubaki ulitokana zaidi na mapenzi yake kwa klabu, familia pamoja na mazungumzo aliyofanya na kocha Ruben Amorim.
“Ninapenda kwa dhati Manchester United, ndiyo maana niliamua kubaki Pia sababu za kifamilia na mazungumzo na kocha vilinifanya nikae,” alisema Fernandes.
Mreno huyo alifichua kuwa alipokea ofa nono kutoka kwa mabingwa wa Saudi Arabia, Al Hilal, lakini akaamua kuikataa licha ya mshahara mkubwa aliokuwa amewekewa mezani.
“Al Hilal walinipenda na mshahara ulikuwa mkubwa sana, lakini niliamua kubaki Uaminifu kwa klabu si kama ulivyokuwa zamani, lakini nilihisi moyo wangu upo hapa,” aliongeza.
Fernandes alikiri kuwa maneno na hisia kutoka upande wa klabu zilimuumiza, akisema inasikitisha kuona mchango wake ukionekana kupuuzwa ilhali yeye huwa tayari kila wakati, anacheza katika hali zote na hutoa kila alicho nacho kwa klabu.
Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa United, wengi wakimpongeza kwa uaminifu wake huku wengine wakihoji msimamo wa uongozi wa klabu kuhusu mustakabali wa nahodha wao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment