BARKER KOCHA MPYA SIMBA SC

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetu sports.

Klabu ya Simba Sc imemtambulisha kocha Steve Barker (57) kukinoa kikosi hicho akichukuwa nafasi ya aliyekuwa Meneja wa timu hiyo Dimitar Pantev alie timuliwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha klabuni hapo.

Kocha huyo rai awa Afrika Kusini ameingoza Stellenbosch kaatika michezo 236, akipata ushindi 88, akipoteza michezo 77 sare 71 huku akiamini kwenye mfumo wa 4-2-3-1.

Ikumbukwe kuwa kocha huyo alishawahi kukutana na waajiri wake wa sasa msimu wa 2024/2025 kwenye nusu fainali mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika na kupoteza 1-0 New Amaan Complex na kutoa sare tasa nchini Afrika kusini.

Timu alizowahi kufundisha nin Pamoja na

-Univesty of pretoria 2008-2014

-Amazuru FC 2018-2016

-Stellenbosch FC 2017-2025


0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments