BAJABER ARUDI KWA KISHINDO, ATOA MGUSO WA KWANZA WA BAO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Kikosi cha Simba SC kimeendelea kurejesha makali yake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3–0 dhidi ya Mbeya City, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo, huku taarifa kubwa ikiwa ni kurejea kwa Mohamed Bajaber aliyefunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Wekundu wa Msimbazi.

Bajaber, ambaye alisajiliwa na Simba huku akitarajiwa kuwa miongoni mwa viungo wabunifu wa timu hiyo, hakupata nafasi ya kung’ara mapema kutokana na majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu, Hata hivyo, kurejea kwake kumeonyesha kile ambacho benchi la ufundi limekuwa likikisubiri.

Kocha alimwingiza uwanjani dakika za mwisho 85' kuchukua nafasi ya Ellie Mpanzu, na kwa mpira wake wa kwanza kabisa (First Touch ) akatikisa nyavu, akihitimisha ushindi wa Simba kwa ustadi wa hali ya juu na kuamsha shangwe kwa mashabiki.

Mabao mengine ya Simba yaliwekwa Kimiani na Morice 28' ,Sowah 38' , Bajaber 85, Simba amefikisha alama 12 nafasi ya tano michezo minne nyuma alama tano dhidi ya JKT mwenye michezo kumi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments