Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa knockout (KO) dhidi ya mpinzani wake Eribo kutoka Nigeria, baada ya kumaliza pambano hilo kwa uusshindi katika mzunguko wa pili.
Pambano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Warehouse, Masaki jijini Dar es Salaam, liliwashuhudia mashabiki wakishangilia kwa shangwe kubwa baada ya Mwakinyo kuonyesha ubora wake kwa kumdhibiti mpinzani tangu mwanzo na hatimaye kumwangusha kwa ngumi kali iliyomlazimisha mwamuzi kumhesabia mpinzani na kusitisha pambano.
Ushindi huo umeleta tabasamu kwa watanzania , limekuwa kama kisasi baada ya timu ya Taifa kupoteza dhidi ya Nigeria mzunguko wa kwanza AfCON sasa raia wa Nigeria kapigika kwenye masumbwi
Kwa ushindi huo, Mwakinyo ameendelea kujiimarisha katika ulimwengu wa ndondi na kuthibitisha kuwa ni miongoni mwa mabondia wanaoipa heshima Tanzania kimataifa, huku wadau wa michezo wakimtaka kupewa mapambano makubwa zaidi ili kuendeleza kipaji chake.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment