BOCCO AREJEA MSIMBAZI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umetangaza kumrejesha aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, John Bocco, katika familia ya klabu hiyo kwa kumkabidhi jukumu la kuwa Kocha wa timu ya vijana akitokea JKT Tanzania, baada ya kumalizika kwa mkataba wake kama mchezaji.

Bocco, ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amepewa dhamana hiyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Simba SC wa kuimarisha programu ya maendeleo ya vijana na kujenga msingi imara wa mafanikio ya baadaye ya klabu.


Mkongwe huyo wa soka la Tanzania anamiliki leseni ya ukocha daraja B ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), sifa inayompa uwezo wa kusimamia mafunzo ya vijana kwa misingi ya kitaalamu na ya kisasa, sambamba na uzoefu wake mkubwa alioupata ndani na nje ya uwanja.

Kupitia uteuzi huo, Simba SC inalenga kuibua na kukuza vipaji vipya vitakavyoweza kujiunga na timu ya wakubwa na timu ya Taifa hapo baadaye.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments