Timothy Lugembe
Mwanakwetusports
Mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, atakosekana uwanjani kwa miezi kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu kufuatia jeraha la mfupa.
Taarifa zinaeleza kuwa Isak alipata jeraha hilo hivi karibuni na kufanyiwa upasuaji siku ya Jumatatu, ambapo madaktari wa klabu wamethibitisha kuwa mchakato wa kupona utaendelea kwa muda mrefu.
Hata hivyo, benchi la ufundi lina matumaini kuwa mshambuliaji huyo ataweza kurejea kucheza kabla msimu huu haujamalizika.
Kukosekana kwa Isak ni pigo kwa Liverpool, hasa ikizingatiwa mchango wake tangu ajiunge na klabu hiyo kama usajili wa rekodi ,t limu italazimika kupanga upya safu ya ushambuliaji katika kipindi hiki wanachomkosa mshambuliaji wao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment