Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kumetokea mvutano mkubwa kati ya timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona kuhusu nyota Lamine Yamal, baada ya Barcelona kutuma taarifa kuwa mchezaji huyo hatacheza mechi za timu ya taifa.
Yamal alifanyiwa matibabu kutokana na maumivu, siku ile ile kambi ya Hispania ilipoanza, bila taarifa kutolewa kwa benchi la ufundi la timu ya taifa.
Shirikisho la Soka la Hispania limesema liliarifiwa usiku huo huo na kuamua kumpa Yamal mapumziko ya siku 7–10, huku kocha De La Fuente akisema ameshangazwa kwa kutopata taarifa mapema.
Yamal sasa atarejea tena uwanjani baada ya wiki mbili ili kuimarisha hali yake ya kiafya.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment