Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ligi kuu nchini England imeendeleza wikendi iliyopita kwa kushuhudiwa michezo tisa iliopigwa viwanja tofauti tofauti ikimalizika Kwa matokeo ya kushangaza.
LIVERPOOL 0-3 NOTTINGHAM
Mchezo ulifanyika uwanja wa Anfield ikishuhudiwa majogoo wakizidi kupoteana kwenye mbio za ubingwa na mwendelezo wa kupata matokeo ya kusuasua msimu huu, mabao ya Nottingham yaliwekwa kimiani na Murillo 33' , Savona 46' na Gibbs-White 78. Matokeo hayo yamewaporosha majogoo mpaka nafasi ya 11 alama 18 huku Nottingham wakipanda mpaka nafasi ya 16 alama 12.
NEWCASTLE 2-1 MAN CITY
Mchezo ulipigwa uwanja wa St James' park ambapo washindani wakuu wengine kwenye mbio za ubingwa Man city wamejikuta wakipoteana na kushindwa kuvuna alama yoyote kitu kilicho ongeza pengo la alama na washindani wake wakuu akiwemo Arsenal, mabao ya Newcastle yalikwamishwa kimiani na Harvey Barnes 63' , 70, bao La kufutia machozi la City likikufungwa na Ruben Dias 68. Matokeo haya yamewaacha City nafasi ya tatu na alama 22 alama Saba nyuma ya vinara Arsenal huku Newcastle wakishikilia nafasi ya 14 alama 15.
Mbio za ubingwa EPL zimezidi kutotabilika baada ya vigogo kutokuwa na mwendelezo wa kupata matokeo ya ushindi , lakini imekuwa neema kwa klabu ya a Arsenal ambayo inazidi kujikita kileleni na kuongeza wigo wa alama na washindani wao, ushindi wa 4-1, dhidi Spurs hapo Jana unawanya kufikisha alama 29 alama sita mbele ya Chelsea anaeshika nafasi ya pili.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment