TUZO ZA AFRIKA KUFANYIKA RABAT MOROCCO

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa hafla ya utoaji wa tuzo za Wachezaji bora barani Afrika kwa mwaka 2025 itafanyika Jumatano ya Novemba 19, 2025, mjini Rabat, Morocco.

Tuzo hizo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutambua na kuthamini mafanikio ya wanamichezo bora wa soka kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, hufanyika kwa ushirikiano na wadau wakuu wa soka barani humo pamoja na wadhamini wakubwa wa mashindano ya CAF.

Miongoni mwa vipengele vitakavyoshindaniwa ni pamoja na Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaume na wanawake, Kocha Bora wa Mwaka, timu Bora ya Taifa ya Mwaka, Klabu Bora ya Mwaka, pamoja na Mchezaji Bora Chipukizi.

Hafla hiyo pia inatarajiwa kuvutia wadau mbalimbali wa soka, wachezaji wakongwe, viongozi wa mashirikisho ya soka, na wapenzi wa mchezo huo kutoka mataifa yote ya Afrika.

CAF imesema maandalizi yanaendelea vizuri na imeahidi kufanya hafla yenye hadhi ya kipekee itakayodumisha utamaduni wa heshima kwa wachezaji na makocha waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka barani Afrika.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments