Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Dirisha la usajili limepata moto mpya baada ya Al Ahli Tripoli ya Libya kurudi kwa nguvu kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili Feisal Salum Fei Toto, wakituma ofa ya dola milioni 2 (takriban Tsh bilioni 4.8) kuelekea Azam FC.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mazungumzo, hii ni ofa ya pili kwa Wa Libya hao baada ya ile ya mwanzo ya dola 800,000 kukataliwa na klabu, Safari hii Tripoli wameweka dhamira ya wazi wako tayari kulipa fedha hizo ili kufunga dili mapema kabla ya dirisha kufungwa.
Zaidi ya hapo, Tripoli wamependekeza kipengele cha sell-on clause cha asilimia 10 endapo Fei Toto atauzwa mbele ya safari Azam watafaidika na asilimia hizo.
Kwa upande wa mchezaji, taarifa zinaeleza kuwa Fei yuko tayari kuanza maisha mapya nje ya Azam akisubiri tu klabu zote mbili kuweka saini za mwisho.
Dili hili likikamilika, litakuwa moja ya uhamisho wakubwa kuwahi kufanywa na klabu ya Tanzania katika miaka ya karibu huku fei akitarajia kukusanya bilioni 10, kwa kusaini mkataba.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment