TPLB YASHUSHA RUNGU KWA WAAMUZI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewasimamisha mwamuzi wa kati Amina Kyando kutoka Morogoro na mwamuzi msaidizi namba mbili Abdalah Bakenga kutoka Kigoma, kwa kushindwa kutafsiri na kusimamia ipasavyo sheria za mchezo wa soka.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa waamuzi hao wameondolewa kwa michezo mitano kwenye orodha ya waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu kutokana na makosa yaliyofanyika katika mchezo kati ya Pamba Jiji FC dhidi ya Singida Black Stars, uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, na kumalizika kwa sare ya bao 1–1.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waamuzi hao walishindwa kuchukua hatua sahihi katika tukio ambapo kipa wa Singida Black Stars alidakia mpira akiwa nje ya eneo la kuminanane bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu, jambo lililotafsiriwa kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za mchezo wa soka.

Aidha, bodi iliongeza kuwa waamuzi hao pia walionekana kushindwa kuumudi mchezo na kukosa kujiamini katika kutoa maamuzi sahihi wakati wa mchezo huo, hali iliyosababisha malalamiko kutoka kwa wadau wa soka.

Hivyo, Amina na Bakenga hawata chezesha michezo yoyote ya Ligi Kuu kwa kipindi cha mizunguko mitano huku wakitakiwa kupitia upya kanuni na taratibu za utendaji wa waamuzi kabla ya kurejeshwa kazini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments