Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno Christiano Ronaldo amethibitisha kuwa kombe la Dunia la mwaka 2026 litakalofanyika kwa ushirika wa nchi tatu ndilo litakuwa la mwisho kwake huku akitarajia kustaafu rasmi ndani ya miaka miwili ijayo.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa utalii 2025 Riyadhi, Saud Arabia. Ambapo alibainisha kuwa michuano hiyo itakayo fanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu Marekani, Mexico na Canada kuwa ndilo litakalo funga ukurasa wake kwenye michuano hiyo mikubwa.
Ronaldo (40), amefanikiwa kushinda ballon d'or mara tano huku shauku yake ikiwa ni kutundika daruga akiwa na mabao 1000 ambapo mpaka sasa ana mabao 953.
Ikumbukwe kuwa Christiano anakwenda kucheza kombe la Dunia la sita lakini hajafanikiwa Kutwaa kombe hilo, je kwa mwaka 2026 atafanikiwa Kutwaa taji hilo na kuacha unyonge mbele ya mpinzani wake Lionel Messi ambaye tayali amekwisha twaa taji hilo, mwaka 2026 ndio utatoa majibu ya hatima yake.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment