Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea imeendelea kuthibitisha ubabe wake katika soka la kimataifa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Barcelona kwenye michuano ya UEFA champions league katika uwanja wa Stamford bridge.
Chelsea waliutawala mchezo eneo la kati huku ubora wa Enzo Fernandez na Reece James eneo la kati ukiwavuruga klabu ya Barcelona, bao la kwanza lilitokana na makosa ya beki wa Barcelona, Jules Kounde aliyerudisha mpira vibaya na kujifunga 27', na kuipa Chelsea uongozi mapema. Makosa hayo yalionekana kuwachanganya kikosi cha Barca na kutoa nafasi kwa wenyeji kutawala mchezo.
Kipindi cha pili The blues walianza kwa kasi na juhudi zao zimelipa dakika ya 55 kupitia kwa Estevao, chipukizi anayetikisa , na kufifisha ndoto za Barca kupata alama darajani.
Dakika ya 73, Delap alikamilisha karamu ya mabao kwa kumalizia kombora safi lililoipa Chelsea bao la tatu na kuwakamilishia usiku wa furaha mashabiki wa The Blues.
Kilicho watoa mchezoni Barcelona ni pamoja na kadi nyekundu alionyeshwa beki wa timu hiyo Ronald Araujo 44' na kuwalazimu kucheza pungufu kwa takribani dakika 50 na kupoteza mchezo huo.
Ushindi huu umeongeza hadhi ya Chelsea kama moja ya timu hatari zaidi duniani kwa sasa, ikiwa na mwendelezo mzuri wa matokeo dhidi ya vigogo wa Ulaya wakiwa wamezifunga timu Bora zaidi Duniani ikiwemo PSG kwenye ubora wake na Jana ilikuwa zamu ya Barcelona kunywa kikombe hicho.
Matokeo ya michezo mingine ni Man city 0-2 Leverkusen, Ajax 0-2 Benfica, Galatasaray 0-1 Union St.Gilloise, Bodoglimt 2-3 Juventus, Dortmund 4-0 Villarreal, Marseille 2-1 Newcastle,Slavia Prague 0-0 Athletic club, Napoli 2-0 Qurabaq.
Hakika Chelsea anadhihirisha kuwa yeye ni bingwa wa Dunia.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment