TANZANIA U17 YAIPIGA DJIBOUTI 11-0, YAENDALEA KUNG’ARA CECAFA

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Timu ya Taifa ya Vijana wa Tanzania U17 imeanza kwa kishindo kwenye michuano ya kufuzu AFCON CECAFA baada ya kuichapa Djibouti U17 mabao 11-0 hapo Jana.

Katika ushindi huo mnono, vijana wa Serengeti Boys walionyesha kiwango cha juu kwa kutawala mchezo mwanzo hadi mwisho ambapo Mabao yalifungwa na Issa Chole, Sadam Hamis, Nhingo Juma, Dismas Athanas na Soann Adam, huku Luqman Ally akiongoza orodha ya wafungaji kwa kutupia mabao sita peke yake.

Ushindi huu unaipa Tanzania matumaini makubwa ya kutinga hatua inayofuata, huku benchi la ufundi likisifu nidhamu na ubora ulioonyeshwa na kikosi hicho chipukizi. Vijana hao wanatarajiwa kuendelea na moto huo katika mechi zao zijazo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments