Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Winga wa Leicester City, Stephy Mavididi, ameonekana kubadili msimamo wake na sasa yuko tayari kuitumikia Timu ya Taifa ya DR Congo (Leopards), baada ya awali kukataa mwaliko wa kuichezea nchi hiyo licha ya kuwa na asili ya huko.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu wa karibu na familia yake, Mavididi anasubiri mwito rasmi kutoka kwa kocha wa taifa ili kujiunga na kikosi hicho, hatua inayotajwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya DR Congo.
Taarifa zinaeleza kuwa kocha wa taifa yuko katika hatua za mwisho kutuma mwaliko rasmi, huku shirikisho la soka la DR Congo likiendelea kufuatilia mwenendo wake klabuni.
DR Congo inatarajiwa kumenyana na mshindi kati ya Jamaica na New Caledonia katika mchezo muhimu wa mchujo kuelekea Kombe la Dunia, na ujio wa Mavididi unatazamwa kama njia ya kuongeza nguvu katika kikosi.
Mashabiki wa soka nchini DR Congo wamepokea taarifa hizi kwa furaha, wakiamini kuwa mabadiliko ya msimamo wa Mavididi yanaweza kuwa sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuimarisha kikosi cha taifa hilo kuelekea mashindano ya kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment