SIMBA NA KAPOMBE WATUPWA NJE YA TUZO ZA AFRIKA, MAYELE AUBEBA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba na nahodha wa kikosi hicho, Shomari Kapombe, wameondolewa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya timu bora na Mchezaji bora wa Mashindano Afrika (CAF Interclub Player of the Year) 2025, hatua inayowafanya Wekundu wa Msimbazi kushindwa kuweka mwakilishi katika hatua ya mwisho ya tuzo hizo.

Wachezaji waliosalia kwenye tatu bora kuelekea kumpata mshindi ni

-Fiston Kalala Mayele – Pyramids FC

-Mohamed Chibi – Pyramids FC

-Oussama Lamlioui – RS Berkane

Hii inaonyesha wazi kuwa Pyramids FC imeweka nguvu kubwa msimu huu, kwa kuingiza wachezaji wawili, huku Berkane ikibaki na mwakilishi mmoja pekee.

Mayele Abeba Afrika Mashariki

Bado kuna mwanga kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kupitia nyota wa DR Congo, Fiston Mayele, ambaye ndiye mchezaji pekee wa ukanda huo aliyesalia katika hatua ya mwisho.

Klabu zilizo salia ni

Mamelod -Afrika Kusini

Pyramid -Egypt

RS Berkane - Morocco

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments