Mwanakwetusports.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewatunuku tuzo maalum za heshima Marais wa nchi tatu za Afrika Mashariki waliotoa mchango mkubwa katika maandalizi ya michuano ya CHAN 2024, iliyofanyika kwa mfumo wa ushirikiano wa kikanda.
Katika tuzo hizo, Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Kenya William Ruto pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, kutambuliwa kwa juhudi zao za kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa ubora unaotakiwa, CAF imeeleza kuwa uongozi wa viongozi hao uliwezesha maandalizi kuwa thabiti, mazingira kuwa salama na mashindano kufanyika kwa kiwango cha juu cha ushindani.
Ushirikiano huo wa mataifa matatu umeonekana kama mfano bora wa kuandaa michuano ya kimataifa barani Afrika, hatua inayoweza kufungua milango zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki kupewa majukumu makubwa ya michezo katika siku zijazo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment