Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timamu mbili kongwe barani Afrika, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), zimefuzu kucheza fainali ya mchujo wa awali wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia Kanda ya Afrika baada ya kupata ushindi muhimu kwenye hatua ya nusu fainali zilizopigwa nchini Morocco.
Nigeria ilijikatia tiketi ya fainali kwa ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Gabon katika mchezo uliolazimika kuongezwa dakika 30 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, Victor Osimhen aling’ara kwa kufunga mabao mawili ya dakika za nyongeza (102’ na 110’), huku Adams (78’) na Ejuke (97’) wakikamilisha karamu ya mabao ya Super Eagles, bao la kufutia machozi la Gabon lilifungwa na Lamina dakika ya 89.
Katika nusu fainali nyingine, Cameroon ilijikuta ikitupwa nje ya mchujo huo baada ya kuchapwa 1-0 na DR Congo, bao pekee likifungwa na nahodha Chancel Mbemba dakika ya 90+1, Ushindi huo wa dakika za mwisho uliwapeleka Congo DR hatua ya fainali, wakitaraji kuikabili Nigeria.
Fainali kati ya Nigeria na DR Congo itapigwa jumapili Novemba 16 2025, nchini Morocco linatarajiwa kuwa pambano la kukata na shoka, huku timu zote zikisaka nafasi muhimu ya kusonga mbele katika safari ya kuelekea Kombe la Dunia.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment