MIEZI MIWILI HADI MITATU BILA CAMARA MSIMBAZI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Golikipa wa timu ya Taifa ya Guinea na klabu ya Simba Pinpin Moussa Camara amefanyiwa upasuaji wa goti nchini Morocco na anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili hadi mitatu.

Camara, alipata majeraha kwenye mchezo wa klabu bingwa hatua ya pili ya Awali dhidi ya Gaborone united ya Botswana ambapo alitolewa kipindi Cha pili , majeraha ambayo yame muweka nje ya uwanja hadi hivi Leo.

Klabu ya Simba ipo kwenye maandalizi kuelekea michezo ya klabu bingwa ambapo watamkosa nyanda huyo , huku kwenye milingoti mitatu akitarajia kusimama Yakoub Suleimani.

Kukosekama kwa Camara ni pengo kwani ni golikipa mwenye uzoefu na michezo mikubwa hata timu ikiwa kwenye presha ya mashambulizi anauwezo wa kutuliza timu pia ni mzuri kwenye uanzishaji wa mashambulizi na anauwezo wa kuchezea mpira kitu kinacho mtofautisha na Yakoub.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments