Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kylian Mbappe ameweka historia mpya ndani ya Real Madrid baada ya kung’ara kwa kiwango cha juu katika ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Olympiacos kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) uliochezwa jana.
Mbappé alifunga mabao manne kwenye mchezo huo, hatua iliyomfanya kuwa mchezaji wa pili tu katika historia ya Real Madrid kufanikiwa kutupia kamba nne kwenye mchezo moja waa UCL. Rekodi hiyo ya kipekee ilikuwa ikishikiliwa na shujaa wa muda mrefu wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Real Madrid walilazimika kupambana kwa nguvu baada ya Olympiacos kuonyesha upinzani mkali, lakini ubora wa Mbappe uliibeba timu hiyo na kuipatia pointi tatu muhimu ugenini, Kila bao lake lilikuja katika wakati muhimu, likibadilisha mwelekeo wa mchezo na kuonyesha kiwango cha juu alichojaaliwa tangu arejee Bernabeu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment