Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hali si shwari katika klabu ya Liverpool baada ya kukumbwa na kipigo kizito cha mabao 3–0 kutoka kwa Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa jana katika uwanja wa Etihad.
Mabao ya City yalifungwa na Erling Haaland, Gonzalez na Doku wakionesha ubabe na ubora mkubwa mbele ya kikosi cha Arne Slots kilichoonekana kupoteza mwelekeo mapema katika mchezo huo.
Kutokana na matokeo hayo, Liverpool imeshuka hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma ya Manchester United ambao sasa wamepanda hadi nafasi ya saba wote wakiwa na alama sawa (alama 18).
Baada ya kipigo hicho Liverpool wanafikilia kumsajili mshambuliaji wa Galatasaray Victor Osmhen wakiwa kwenye harakati sawa na klabu ya Chelsea na Man utd.
Huu unakuwa ni mchezo wa tano wanapoteza kwenye ligi huku mashabiki wa majogoo wameanza kuonesha wasiwasi kuhusu mwenendo wa timu hiyo, huku baadhi wakimtaka kocha kufanya mabadiliko makubwa kwenye safu ya ulinzi na kiungo ambavyo vimeonekana kuwa dhaifu msimu huu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
.



Post a Comment