KUTOANZA NA MSHAMBULIAJI HOJA KIPIGO KWA MNYAMA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba Sc imepokea kichapo Cha 1-0, kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi klabu bingwa dhidi ya Petro Atletico kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Katika mchezo huo wadau na mashabiki wa klabu ya Simba walishangazwa na jinsi Meneja wa klabu hiyo Pantev kuanza bila mshambuliaji halisia( namba Tisa) ambapo ilishudiwa washambuliaji wa timu hiyo wote watatu Sowah, Mukwala na Mwalimu wakianzia mabao ndefu na timu kuanza na viungo Wengi.

Lengo la kocha kuanza na viungo Wengi ilikuwa ni kutawala umiliki wa mpira lakini licha ya mkakati huo Bado hawakufanikiwa na badala yake walijikuta wakishindwa kumiliki mchezo na kuukosa nafasi za wazi zilizo wanyima ushindi.

Takribani nafasi tatu za wazi za kuandika mabao zilikoswa na viungo wa timu hiyo ikiwemo nafasi ya kipindi Cha kwanza ya Morice Abraham na Ile ya Mpanzu, kitu ambacho kimezua maswali huenda wakingekuwepo washambuliaji halisia wangeweza kusaidia kukwamisha mpira kimiani.

Kwa sasa Simba wamekumbwa na ugumu wa kupata matokeo kwenye dimba la Mkapa toka msimu huu wa mashindano uanze ambapo katika michezo yake mitatu ya klabu bingwa iliyopingwa Simba hawajapata ushindi uwanja wa nyumbani wakifungwa mchezo mmoja na kutoa sare michezo miwili.

Mchezo unaofuata Simba watakuwa ugenini dhidi ya Stade Melien mchezo utakaopigwa Novemba 28, 2025 .

Swali ni je , klabu itafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali kama ilivyokuwa tamaduni Yao, ukizingatia michuano hii timu hulinda kutumia zaidi viwanja vya nyumbani, hii haimaanishi kuwa Simba wametoka ila wamesalia na michezo mitano na kutokana na kupata kwao matokeo ugenini huenda wakapindua meza mchezo wa Novemba 28 utatoa taswira kuhusu mwelekeo wa klabu hiyo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments