Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya KMC imejikuta ikikumbana na matokeo mabovu mara baada ya kupoteza mchezo wa Jana dhidi ya Yanga kwa bao 4-1, kwenye uwanja wa KMC complex na kufikisha idadi ya michezo sita wakiwa wameshinda mmoja na kufungwa mitano.
Timu hiyo inaburuza mkia ikiwa na alama tatu wakiwa wamefungwa goli mbili na kufungwa bao kumi, kinachofikirisha ni kuwa klabu Ina moja ya kocha mahiri (Marcio Maximo) kutokea nchini Brazili ambae lishawahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania lakini isivyo bahati mambo yamemuendea alijojo klabuni hapo.
Michezo mingine matokeo yake yalikuwa hivi
Pamba Jiji 1-1 Singida black stars
JKT Tanzania 1-2 Simba SC
Namungo 1-1 Azam
Mpaka sasa kwenye ligi kuu NBC Tanzania Bara Simba ndio timu pekee iliyoshinda kwa asilimia miamoja baada ya kucheza michezo mitatu na kushinda yote, huku wakiwa nafasi ya pili nyuma Yanga wenye alama 10 na mchezo mmoja mbele ya Simba.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment