Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa soka duniani wanatarajia burudani ya aina yake leo Jumamosi Novemba 8 , ambapo ligi mbalimbali zinatarajiwa kushuhudia michezo kadhaa ya kuvutia.
Katika Ligi Kuu ya England, macho yote yatakuwa kwenye dimba la Tottenham Hotspur saa 15:30, ambako Tottenham Hotspur watapambana na Manchester United katika mchezo unaotabiriwa kuwa na ushindani mkubwa,mbungi nyingine za EPL zitapigwa saa 18:00 ambapo Everton FC watamenyana na Fulham FC, huku West Ham United wakivaana na Burnley FC. Usiku, saa 23:00, Chelsea FC watakuwa wenyeji wa Wolverhampton, katika pambano linalotarajiwa kuamua nafasi ya timu hizo katika nusu ya juu ya msimamo.
Kwa upande wa Tanzania, macho ya Watanzania wengi yatakuwa Meja Isamuhyo saa 19:00, wakati JKT Tanzania FC watakapokutana uso kwa uso na mabingwa watetezi Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, Mapema saa 16:00, Pamba Jiji FC watawakaribisha Singida Black Stars.
Nchini Ujerumani, mashabiki wa Bundesliga hawatabaki nyuma Saa 17:30, Leverkusen wataikaribisha Heidenheim, huku Union Berlin wakivaana na Bayern Munich , Mchezo mwingine utakaovutia ni kati ya Hamburger SV dhidi ya Borussia Dortmund saa 17:39.
Ligi ya Hispania (La Liga) nayo itakuwa na burudani saa 18:15, Sevilla FC wakiikaribisha Osasuna UD, kabla ya Atletico Madrid kupepetana na Levante saa 20:30.
Italia nayo haitabaki nyuma, ambapo Juventus watawakaribisha Torino FC saa 20:00 katika Derby della Mole, huku AC Milan wakiwa ugenini dhidi ya Parma FC saa 22:45.
Michezo mingine ni pamoja na Olympique Marseille dhidi ya Stade Brest (Ufaransa, saa 19:00), AS Monaco wakivaana na RC Lens saa 23:05, na Santa Clara wakipambana na Sporting CP ya Ureno saa 23:30.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment