KINDA ARSENAL AWEKA HISTORIA ULAYA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Klabu ya Arsenal imeweka historia mpya usiku wa UEFA Novemba 4, 2025, baada ya kinda wao Max Dowman (miaka 15 na siku 308) kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kushiriki mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

Dowman aliingia uwanjani kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Leandro Trossard wakati Arsenal ikiibuka na ushindi wa mabao 3–0 dhidi ya Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech.

Kuingia kwake kulitengeneza ukurasa mpya katika historia ya soka barani Ulaya, baada ya kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Youssoufa Moukoko wa Ujerumani, ambaye aliichezea Borussia Dortmund akiwa na miaka 16 na siku 18.

Mchezo huo pia uliendeleza rekodi nyingine ya kuvutia kwa Arsenal, ambayo sasa imefikisha ushindi wa michezo 10 mfululizo na clean sheet nane mfululizo rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na klabu hiyo tangu mwaka 1903.

Kocha mkuu wa Arsenal alimsifu Dowman kwa ujasiri wake uwanjani licha ya umri mdogo, akisema hatua hiyo ni mwanzo wa safari ndefu kwa mchezaji huyo chipukizi ambaye anatajwa kuwa na kipaji kikubwa cha kipekee ndani ya klabu hiyo.

Arsenal imebakia nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich wakiwa na alama sawa (12) huku wakiwa wameshinda michezo yote minne waliyocheza.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments