KAULI YA MAGUFULI KWA SIMBA NA MAFANIKIO YA SOKA NCHINI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

"Nitafurahi siku Moja mtakapo niita hapa nije kukabidhi kombe la Afrika lililo chukuliwa na timu yoyote katika nchi yetu" alisema Hayati Dk. John Magufuli Rais wa awamu ya Tano katika dimba la Benjamin Mkapa, mei 20, 2018.

Magufuli, alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kukabidhi ubingwa kwa timu za Tanzania zilizofanya vizuri ikiwemo Simba Sc, Serengeti boys na timu ya Taifa ya wanawake wanaoishinkwenye mazingira magumu walio shika.nafasi ya pili kombe la Dunia nchini Urusi.


Katika mchezo huo Simba walipoteza bao 1-0 dhidi ya Kagera sugar huku Dk.Magufuli akizipongeza timu zote kwa kucheza vizuri huku akishindwa kuvutiiwa na kiwango cha klabu ya Simba kuelekea michuano ya kimataifa ambapo alinukuliwa akisema kauli yenye mwiba mchungu kwa Simba lakini chachu ya mafanikio hadi hivi Leo.

"Kwa mpira nilio uona Leo hamuwezi mkachukua kombe la Afrika, nilazima tubadilike".


Hakika kauli hiyo iliwaamsha Simba na kubadilika na kiuchezaji ambapo walifanikiwa kufika hatua ya robo fainali mara kadhaa, Kitu ambacho kili waamsha watani zao Yanga , nao kuanza kufanya vizuri wakifuzu hatua ya makundi mara tatu mfululizo huku klabu za Azam na Singida nazo ziki fuata nyayo za wakubwa wao.

Magufuli hakuamini kwenye kushindwa aliamini kwenye ushindi siku zote katika sekta tofauti tofauti za kimaendeleo, na siku hiyo aliwaamsha Wana michezo nchini na historia ikaanza kujengwa chini ya uongozi wa Wallace Karia raisi wa TFF.

Aidha, aliwapa Simba nguvu kwa kauli yake ya matumaini akisema " Nimatumaini ushindi huu utasaidia kuleta kombe la Afrika hapa ilikusudi mje mnikabidhi kwa siku nyingine"

Kwa kutambua ubora wa klabu ya Simba kwa kipindi kile Hayati Magufuli aliwaomba wakawe wakwanza kutoka Tanzania kuleta kombe la Afrika. " Kwahiyo niwaombe Simba mkawe wa kwanza kuleta kombe la Afrika hapa Tanzania".

Ilibaki punje tu klabu hiyo ililete kombe Hilo nchini baada ya kufika hatua ya Fainali dhidi ya Berkane, isivyo bahati walipoteza kwa kufungwa Jumla ya bao 3-1 na kupoteza kikombe hicho.

Lakini mpaka sasa inaaminikankuwa Simba ndio msingi wa klabu nyingine kutoka hapa Tanzania kufanya vizuri kimataifa pia klabu imesaidia kutoa fursa kwa nchi kuwa na uwakilishi wa vilabu vinne kutokana na kufany vizuri kwenye michuano hiyo ikichagizwa na kufika hatua ya robo fainali mara kwa mara.


Itoshe kusema nyuma ya mafanikio ya Klabu zetu kimataifa kuna mchango mkubwa wa Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli Raisi wa awamu ya Tano nchi Tanzania, hakika alifanya mengi mazuri na Leo hii wanamichezo tunakumbuka jitihida na ushauri wako kuelekea mafanikio tuliyo fikia hivi Leo.

'pumzika kwa amani shujaa wetu , wanamichezo na wa Tanzania wote tunakukumbuka hakika wewe ndio chanzo Cha mafanikio katika soka letu'.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments