Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kylian Mbappe ameendelea kuthibitisha hadhi yake kama mmoja wa washambuliaji bora wa kizazi hiki baada ya kufikisha magoli 400 katika maisha yake ya soka la ushindani, rekodi ambayo inamfanya kuwa mchezaji ndogo zaidi katika karne ya 21 kufikia alama hiyo ya kihistoria.
Takwimu hizi si za kawaida, na ndizo zinazoonyesha ukubwa wa safari yake mpaka sasa hivi ndivyo magoli yake yanavyogawanyika katika klabu na timu ya taifa:
Paris Saint-Germain (PSG): 256
Real Madrid: 62
France : 55
AS Monaco: 27
Kwa jumla ya mabao haya, Mbappe anaendelea kupanda ngazi ya mastaa wakubwa duniani, huku kila wiki akionekana kuongeza historia mpya katika soka la dunia, Kasi, ustadi, na uwezo wake wa kumalizia nafasi vinaendelea kumfanya awe tishio kwa mabeki na magolikipa popote anapocheza.
Ikiwa ataendelea na kiwango hiki, sio tu kwamba ataandika rekodi mpya, bali anaweza kubadili kabisa ramani ya rekodi za ufungaji barani Ulaya kwa miaka mingi ijayo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment