HAWA HAPA WASHINDI CAF TUZO ZA CAF 2025 MZIZE NAE NDANI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Tuzo za CAF 2025 zilizosubiriwa kwa hamu hatimaye zimefanyika mjini Rabat nchini Morocco siku ya Jana Novemba 19, 2025.

WASHINDI WA TUZO



Achraf Hakimi

Mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Morocco ameibuka mchezaji Bora wa kiumen kutokana na mafanikio aliyoyapata yakijumuisha mshindi wa kombe la ulaya UEFA champions league, mshindi wa kikombe cha ligi kuu Ufaransa, kufika hatua ya fainali club world Cup pia ameiongoza Morocco kufuzu kombe la Dunia.

Fiston Mayele

Mchezaji wa Pyramid na timu ya taifa ya Congo DR amefanikiwa Kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ndani kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Bara la Afrika, Mayele akiibuka mfungaji wa ligi ya mabingwa barani Afrika , pia kaiongoza pyramid Kutwaa klabu bingwa kwa mara ya kwanza akiwa ni sehemu na muhimili mkubwa wa mafanikio ya timu hiyo.


Clement Mzize

Ni mchezaji wa Yanga Africans na timu ya taifa ya Tanzania amefanikiwa Kutwaa tuzo ya goli bola la mwaka aliloweka kimiani kwenye mchezo dhidi ya Tp mazembe kwenye dimba la Benjamin Mkapa jiji Dar es laam.

Yassine Bounou

Ni golikipa wa Al Hilal ya saud Arabia na timu ya taifa ya Morocco ndiye amefanikiwa Kutwaa tuzo hiyo kwa mwaka 2025.


Pyramid

Ni timu kutokea nchini Misri ambayo kwa mara ya kwanza imetwaa taji la klabu bingwa na kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi, kutokana na kiwango bora walicho onyesha mbele ya vigogo kama Al Ahaly na Mamelod kumewafanya kuwa na upekee na kutunukiwa kuwa klabu bora ya mwaka.

Hakika walioupata tuzo wamestahili kutokana na jitihada walizo zifanya je, msimu ujao watajirudia wale wale au kutakuwa na maingizo mapya? muda utaongea.

0767915474

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments