Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika ulimwengu wa soka mashujaa huzaliwa na kupitia misukosuko, pia Kauli ya dhahabu ili ing’ae hupitia kwenye moto,bkauli hii imethibitika na safari hii ni kupitia Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube.Katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa jana, Novemba 22, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Yanga SC ilipata ushindi mwembamba wa 1–0 dhidi ya Far Rabat ya Morocco, pongezi kwa bao pekee lililofungwa na Dube bao ambalo limeonekana kuwa uthibitisho wa kauli kuwa wakati wa Mungu ni wakati sahihi.
Dube amekuwa akipitia kipindi kigumu cha ukame wa mabao, akikosakosa nafasi nyingi za wazi na kukumbana na maneno mazito kutoka kwa baadhi ya mashabiki Lakini jana, muda wake ulifika, “Mwana mfalme” huyo alisimama imara, na kuzamisha mpira wavuni akiwapa Wananchi pointi tatu muhimu kwenye safari yao ya Afrika.
Yanga wanatarajiwa kuanza safari kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa pili dhidi ya Js kablyie utakao pigwa Novemba 28 mwaka huu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment