Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya Congo DR imeweka hai matumaini yake ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi muhimu wa mabao 4–3 kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya 1-1 dakika 120 dhidi ya Nigeria, katika fainali ya play off iliopigwa mjini Rabat nchini Morocco.
Kwa ushindi huo, Congo sasa imefuzu kucheza Inter-Continental Confederation Play-offs, hatua ambayo inaweza kuirejesha nchi hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili katika historia yake tangu iliposhiriki kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1974.
Congo yadhibiti mpira, Nigeria yatetereka
Mchezo ulishuhudia kasi na ubunifu mkubwa kutoka kwa Congo, ambao walionyesha nidhamu ya hali ya juu katika safu ya ushambuliaji na kiungo, Ushindi huo umeonekana kama uthibitisho wa maendeleo makubwa ya soka nchini humo, huku benchi la ufundi likisifiwa kwa maandalizi na mbinu zilizowapa matokeo dhidi ya moja ya timu zenye historia kubwa barani Afrika.
Nigeria, ambayo ilitarajiwa kuwa na udhibiti wa mchezo kutokana na uwepo wa nyota wao kama Victor Osimhen, ilijikuta ikiwa nyuma ya matokeo muda mwingi kutokana na makosa ya kiufundi na kukosa umakini katika safu ya ulinzi, Licha ya juhudi zao kurejea kwenye mchezo, juhudi hizo hazikuweza kuwapa ushindi.
Ndoto ya Nigeria yagubikwa na giza
Super Eagles sasa wamekosa Kombe la Dunia mara ya pili mfululizo, jambo ambalo limesababisha mjadala mpana miongoni mwa wadau wa soka nchini humo, Matumaini ya mashabiki Nigeria ilikuwa ni kuona kizazi cha sasa kikiongozwa na Osimhen kikirudi kwenye ramani ya dunia lakini isivyo bahati yameingia dosari.
Historia mpya ya Congo yazidi kukaribia
Kwa upande wa Congo, matokeo haya yamepokelewa kwa shangwe na matumaini mapya, Ikiwa itafaulu kwenye hatua ya play-offs, taifa hilo litajiandikia historia ya kipekee katika kipindi cha zaidi ya nusu karne.
Congo sasa inabaki hatua moja tu kutimiza ndoto ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa zaidi ya miaka 50 na kwa jinsi walivyocheza, inaonekana hawako tayari kurudi nyuma.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment