Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Al Ahly ya Cairo, Misri, imeingia katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa Pyramids Fiston Mayele wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari, kwa mujibu wa taarifa zinazoripotiwa kutoka nchini Misri.
Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa Al Ahly iko tayari kumweka mezani mshahara mnono unaofikia takribani Tsh milioni 180 kwa mwezi, ikiwa itafanikiwa kumshawishi nyota huyo kujiunga nao.
Mayele, ambaye ameendelea kung’ara katika siku za karibuni, amekuwa kivutio cha vilabu kadhaa vinavyotafuta safu ya ushambuliaji yenye tija huku alifanya vizuri na msimu akitwaa tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment