Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezaji nyota wa kimataifa wa Morocco, Hakim Ziyech, ametua rasmi katika klabu ya Wydad Casablanca baada ya kufikia makubaliano ya kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Afrika kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Ziyech (32), ambaye amewahi kuchezea klabu za Chelsea ya England na Ajax Amsterdam ya Uholanzi, amesaini kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Al-Duhail ya Qatar.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya michezo, Ziyech amekubali kujiunga na Wydad ili kuendeleza kipaji chake nyumbani Morocco, akitarajiwa kuwa chachu muhimu kwenye kikosi hicho kinachopania kurejea kwenye ubora wake wa Afrika.
Ndani ya Wydad, Ziyech ataungana na Stephane Aziz Ki, kiungo wa zamani wa Yanga SC ya Tanzania, ambaye pia amesajiliwa hivi karibuni na klabu hiyo.
Ziyech alikuwa sehemu ya kikosi cha Ajax Amsterdam kilichofika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/2019, akifunga bao muhimu dhidi ya Real Madrid katika hatua ya 16 bora kabla ya kutolewa na Tottenham Hotspur.
Usajili wake ndani ya Wydad unatazamiwa kuleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa, hasa kwa vijana wa Morocco wanaotamani kuona timu yao ya nyumbani ikirudi kutamba katika soka la kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment