Emakulata Msafiri
Mwanakwetusports
Ecua Celestin na Lassine Kouma wamejiunga na kikosi cha ya yanga kilichosafiri kuelekea Malawi wakitokea kwenye majukumu ya timu yao ya Taifa ya CHAD. Kuwasili kwao kumeongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na kiungo cha Yanga kwani wote wawili wanajulikana kwa kucheza kwa nidhamu na juhudi kubwa wanapokuwa uwanjani.
Safari hii ni sehemu ya maandalizi ya mchezo muhimu wa kimataifa dhidi ya Silver Strikers mchezo unaotarajiwa kuvuta mashabiki wengi kutokana na ushindani wa klabu hizi mbili.
Kikosi cha Yanga kimeonesha kiwango kizuri kwenye mechi zao za hivi karibuni na morali ya wachezaji iko juu. Benchi la ufundi limeahidi kupambana kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri ugenini ili kujihakikishia nafasi nzuri kwenye michuano hii.
Tarehe ya Mechi: Jumamosi, Oktoba 18, 2025,
Uwanja: Bingu National Stadium
Muda: Saa 9:00 Jioni kwa saa za Malawi (Saa 10:00 Jioni kwa saa za Tanzania)
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kasi na ushindani mkubwa kwani Silver Strikers ni timu inayojulikana kwa kutumia vizuri faida ya uwanja wa nyumbani. Hata hivyo Yanga imejipanga kikamilifu ikiwa na malengo ya kuonyesha ubora wake na kuendeleza rekodi nzuri ya matokeo nje ya nyumbani.
Mashabiki wote wa Yanga ndani na nje ya Tanzania wanahimizwa kuendelea kuipa sapoti timu kwa sala hamasa na kueneza taarifa nzuri kuhusu klabu. Uongozi wa klabu umeahidi kupigania heshima ya Jezi ya Njano na Kijani hadi dakika ya mwisho.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment