WITO WA KUINGA MKONO JKT QUEENS KIMATAIFA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, amewataka Watanzania kuiunga mkono timu ya wanawake ya JKT Queens, ambayo inajiandaa kuwakilisha taifa pamoja na Ukanda wa CECAFA katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa soka la wanawake.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upangaji wa makundi lililofanyika jijini Cairo, nchini Misri, Meja Jenerali Mabele alisema timu hiyo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote kwani ni mwakilishi pekee kutoka Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya kimataifa.

JKT Queens imepangwa Kundi B likiwa na miamba mikubwa ya soka la wanawake barani humo ikiwemo bingwa mtetezi TP Mazembe kutoka DR Congo, Asec Mimosas ya Ivory Coast, na Gaborone United kutoka Botswana.

Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa wanawake inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 8 hadi Novemba 21, 2025, ambapo jumla ya timu nane (8) zitachuana kuwania taji hilo lenye hadhi ya juu zaidi katika soka la wanawake barani Afrika.

Meja Jenerali Mabele alisisitiza kuwa JKT Queens inaenda kupambana kwa niaba ya Watanzania wote, akiwataka mashabiki kuonyesha uzalendo kwa kutoa sapoti ya hali na mali ili timu hiyo iweze kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya taifa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments