Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Manchester United imeendelea kuzua maswali baada ya matokeo yasiyoridhisha chini ya kocha Ruben Amorim, ambaye hadi sasa ameiongoza timu hiyo kwenye michezo 50 bila mafanikio makubwa.
Katika michezo hiyo, Amorim ameshinda mechi 20 pekee, akatoa sare 9 na kufungwa michezo 21 takwimu zinazoonesha hali ya sintofahamu ndani ya Old Trafford Ushindi wa hivi karibuni wa mabao 2–0 dhidi ya Sunderland ulionekana kama mwanga mdogo katika giza nene, lakini bado haujaweza kufuta mashaka ya mashabiki.
Kwa klabu yenye historia kubwa kama Manchester United, kushinda chini ya nusu ya michezo ni jambo linalotia wasiwasi Wadau wa soka wanahoji iwapo Amorim bado ana uwezo wa kuirudisha timu hiyo kwenye hadhi yake ya zamani kama “mashujaa wa Ulaya.”
Huku presha ikiongezeka kutoka kwa mashabiki na wachambuzi, swali linalobaki ni moja, Je, Manchester United inapaswa kuendelea kumuamini Ruben Amorim, au ni wakati wa kutafuta sura mpya kuleta matumaini mapya Old Trafford?
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment