Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 47 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) uliofanyika mjini Kinshasa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, ameonesha matumaini makubwa kuwa soka litakuwa nguzo ya kuimarisha umoja na mshikamano barani Afrika.
Kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri Mkuu Judith Suminwa Tuluka, Rais Tshisekedi alitoa pongezi kwa Rais wa CAF, Patrice Motsepe, akimsifu kwa uongozi wenye dira na juhudi za kuinua hadhi ya soka la Afrika.
Vilevile, alituma shukrani kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Rais wake Gianni Infantino kwa mchango wao katika kukuza soka barani humo, hususan kwenye maeneo ya utawala, miundombinu na uwezeshaji wa vijana na wanawake.
Aidha, CAF imeweka kipaumbele kipya kwenye maendeleo ya soka la wanawake chini ya Bestine Kazadi kutoka Congo, ambaye alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais anayesimamia sekta hiyo, Hatua hii imeelezwa kama njia bora ya kuhakikisha usawa wa kijinsia na kukuza vipaji vinavyochipukia kote barani Afrika.
Rais Tshisekedi alisisitiza kuwa soka ni zaidi ya mchezo ni lugha ya umoja , Michezo, hasa soka, imekuwa nguzo muhimu ya kuleta amani na mshikamano miongoni mwa mataifa Mfano halisi ni michuano ya AFCON ambayo huwaleta pamoja wachezaji na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali bila kujali tofauti zao.
Wakati wa mashindano hayo, watu hutanguliza urafiki na heshima kuliko migawanyiko, jambo linalosaidia kupunguza mvutano na kukuza undugu wa Kiafrika Kwa maneno mengine, michezo ni daraja la amani linalounganisha bara zima.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment