Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limezindua rasmi mpira mpya utakaotumika kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2026, ujulikanao kama “Trionda.” Jina hilo limetokana na neno la Kihispania linalomaanisha mawimbi matatu, likiwa ishara ya ushirikiano wa mataifa matatu yatakayoandaa mashindano hayo Marekani, Canada na Mexico.
Mpira huo unajumuisha rangi tatu kuu, nyekundu, kijani na bluu, zenye kuwakilisha mataifa hayo matatu. Pia, umebeba alama maalum kama nyota ya Marekani, maua ya lotus kwa Canada, na mamba kwa Mexico.
“Trionda” imeboreshwa kwa teknolojia ya kisasa inayowezesha kutuma taarifa moja kwa moja kwa waamuzi ili kurahisisha utambuzi wa faulo, mpira wa mkono, au mchezaji aliyegusa mpira.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alisema mpira huo ni ishara ya umoja na ushirikiano wa kipekee kati ya nchi watatu wenyeji wa Kombe la Dunia 2026.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment