Samson kalekwa
Mwanakwetu Sports
Baadhi ya vilabu vya soka la wanawake nchini vimewasilisha barua rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), vikiiomba kufanyika kwa uchunguzi kuhusu uhalali wa jinsia ya mshambuliaji wa Kimataifa wa klabu ya Yanga Princess, Jeanine Mukandayisenga Raia wa Rwanda.
Vilabu hivyo vinataka kujiridhisha kama mchezaji husika anatimiza vigezo vya kushiriki katika ligi ya wanawake kulingana na kanuni na taratibu zilizowekwa.
Kutokana na ombi hilo, kuna uwezekano TFF ikaamua kutoa zuio la muda kwa mchezaji huyo kushiriki michezoni hadi uchunguzi kamili ukamilike au makubaliano ya pamoja yafikiwe kati ya pande husika — TFF, Yanga Princess, na vilabu vilivyowasilisha hoja hiyo.
Iwapo TFF itachukua hatua hiyo, itakuwa ni uamuzi wa kisheria na unaoendana na miongozo ya FIFA, ambayo inapiga marufuku mchezaji wa jinsia tofauti kushiriki katika ligi isiyo ya jinsia yake. Tukio kama hilo huchukuliwa kama udanganyifu wa kimashindano, unaoweza kupelekea adhabu kwa mchezaji, klabu au shirikisho husika.
Ni muhimu TFF kushughulikia suala hili kwa umakini, kwani kupuuza malalamiko yaliyowasilishwa rasmi kunaweza kuleta athari za kisheria na kiutawala endapo tuhuma hizo zitathibitika.
Kwa mtazamo wa kiuchambuzi wa michezo, hatua ya TFF kuweka zuio la muda itakuwa ya busara na yenye kulinda heshima ya ligi ya wanawake, pamoja na taswira ya vilabu vyote vinavyoshiriki.
Post a Comment