TAIFA STARS YAPOTEANA MARA YA TATU MFULULIZO

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeendelea kuwa na mwenendo mbaya baada ya kuchapwa mabao 2–0 na Iran katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Rashid, mjini Dubai.

Katika mchezo huo, Iran ilionyesha ubabe tangu mapema na kupata bao la kwanza dakika ya 17 kupitia Hosseinzadeh aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, Dakika tisa baadaye, Mohebi aliongeza bao la pili na kuifanya Stars kuonekana kuzidiwa katika maeneo mengi ya uwanjani.

Huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Taifa Stars kupoteza, huku ikiwa haijapata ushindi katika mechi sita zilizopita, ikipokea vipigo vinne na sare mbili pekee, huku ikiwa haifunga goli lolote kwenye michezo yake mitatu iliyopita kitu kinacho acha maswali kwa mashabiki wa Stars.

Matokeo haya yanaongeza presha kwa benchi la ufundi la Stars, ambalo sasa linapaswa kurekebisha mapungufu kabla ya kurejea kwenye michezo mingine ya kimataifa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments