Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imeendelea kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi baada ya kutangaza rasmi kumleta Vitomir Vutov (53), raia wa Bulgaria, kuwa kocha mpya wa makipa klabuni hapo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na klabu hiyo, Vutov amejiunga na benchi la ufundi linaloongozwa na Meneja Mkuu Dimitar Pantev, akisaidiwa na Byoko Kamenov wote wakiwa raia wa Bulgaria.
Kocha huyo mpya tayari ameanza rasmi majukumu yake katika kambi ya Msimbazi, ambapo atakuwa akifanya kazi ya kuwanoa makipa wa timu hiyo ili kuhakikisha wanakuwa katika ubora wa hali ya juu.
Ujio wa Vutov unatajwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa Simba SC wa kuhakikisha wanapata uimara zaidi katika safu ya ulinzi, hususan eneo la mlindamlango, ambalo limekuwa likipewa kipaumbele katika maandalizi ya msimu huu.
Viongozi wa klabu hiyo wamesema wana imani kubwa na benchi jipya la ufundi lenye linalo ongozwa na wa Bulgaria, wakiamini litasaidia kurejesha ubabe wa wekundu hao katika michuano ya ndani na kimataifa.
Simba SC kwa sasa ipo katika maandalizi ya michezo yake ijayo ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mashabiki wakingoja kwa hamu kuona matunda ya mabadiliko haya mapya katika benchi la ufundi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment