AZAM ,SINGIDA TAA YA KIJANI SHIRIKISHO
Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashindano ya klabu bingwa na shirikisho yameendelea kutimua vumbi katika hatua ya awali ya pili ambapo timu tano zinaipeperusha bendera ya Tanzania huku matumaini ya kupelekwa timu nne hatua ya makundi ikiwa kubwa .
NSINGIZINI HOTSPURS 0-3 SIMBA SC
Mchezo huu umepigwa nchini Eswatini katika dimba la Somhololo ambapo mnyama amedhihirisha ubora wake ifikapo michuano ya kimataifa baada ya kuibuka na ushindi katika ardhi ya ugenini huku ule mpira wakuvutia ambao mashabiki wa Simba waliukumbuka ulionekana kurejea chini ya Meneja Pantev, walio pelekea msiba kwa nsingizini ni Wilson Nangu 45+2' na kibunDenis 83', 90. Simba wamecheza mpira mzuri na wakuvutia na timu imeonekana kuimarika kiuchezaji na meneja Pantev ameonekana kumtambulisha soka la ushambuliaji baada ya kuanza na kiungo mkabaji mmoja huku waliobaki wakiwa washambuliaji.
SILVER STRIKERS 1-0 YANGA
Klabu ya Yanga wamekubali kichapo wakiwa ugenini nchini Malawi katika dimba la kipigo ambacho kimeondika na kocha mkuu wa klabu hiyo Romain Folz, ni kwa muda mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakilalamika kuhusu aina ya uchezaji wa kocha huyo na rasmi kilio chao kimejibiwa baada ya klabu kuachana na kocha huyo, kwa sasa klabu ipo mbioni kutafuta mwalimu mpya, Yanga wanahitaji kushinda kwa ushindi wa tofauti ya bao mbili au zaidi ili wafuzu Moja kwa Moja.
KMKM 0-2 AZAM FC
Mchezo huu uliopigwa katika dimba la New Amaan Cmpex Visiwani Zanzibar ambapo Wanalamaba lamba wameingiza mguu mmoja hatua ya makundi shirikisho baada ya kuwatandika ndugu zao kutoka Visiwani Zanzibar, msimu huu Azam wamedhamiria kufika hatua za mbali kimataifa na Hilo limeonekana kuanzia kwenye usajili wa wachezaji mpaka benchi la ufundi kitu ambacho kimeanza kuwalipa sherehe ya wanalambalamba ilichangiwa na mabao ya Kitambala na Msindo, Azam wanahitaji sare au ushindi wa aina yoyote ili kutinga makundi.
FLAMBEAU 1-1 SINDIDA BLACK STARS
Mchezo uliopigwa dimba la Intwari nchini nchini Burundi ambapo Singida wameonyesha ukomavu chini ya kocha wao Gamond kwa kupata sare ugenini, ikumbukwe kuwa timu hizi zote ni ngeni katika mashindano haya huku Black stars wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kusonga mbele kwa faida ya uwanja wa nyumbani, bao la walima alizeti likiwekwa kimiani na Clatous Chama na kuwapa matumaini black stars kusonga mbele , black stars wanahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya bila kufunguna ili kufuzu hatua inayofuata.
Huenda historia ikaandikwa kwa timu nne kutoka Tanzania kutinga hatua ya makundi kwa pamoja kitu ambacho hakijawahi kufanyika , haya ni mafanikio makubwa kutokana na uwekezaji wa hali ya juu na uongozi imara katika vilabu hivi kama timu zote zitafuzu makundi kutaongeza ubora wa ligi na wachezaji wengine watavutiwa kuja kuchezea Tanzania.
Michezo ya marudiano inatarajiwa kupigwa oktoba 25 na 26 huku Simba na Azam wakiwa na asilimia 90 ya kufuzu makundi huku Yanga na Singida wakihitajika kutumia mbinu na maarifa makubwa ili kujinasua na mtego wa kuondoshwa kwenye mashindano.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.




Post a Comment