SIMBA NA KAPOMBE NDANI KUMI BORA TUZO BARANI AFRIKA Timothy Lugembe,

 

Mwanakwetusports.

Shirikisho la mpira barani Afrika CAF limetangaza vonyang'anyiro vya tuzo mbali mbali ikiwemo timu Bora na mchezaji Bora wa mwaka 2025 ambapo klabu ya Simba na nahodha wake wameingiza kwenye kumi wanaowania tuzo hizo.

Klabu ya Simba SC imepata nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa msimu uliopita ikifanya vizuri kwenye mashindano ya shirikisho kwa kufika hatua ya fainali ikipoteza mbele ya Berkane.

Timu nyingine zilizoteuliwa ni Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates na Stellenbosch FC kutoka Afrika Kusini, Asec Mimosas ya Ivory Coast, CS Constantine na CR Belouizdad kutoka Algeria, pamoja na Al Hilal Omdurman ya Sudan.

Katika upande wa wachezaji, Tanzania imepata heshima kupitia nahodha wa Simba SC, Shomari Kapombe, ambaye ametajwa miongoni mwa wachezaji 10 bora wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Afrika 2025 (kwa wachezaji wa ndani ya Afrika).

Kapombe ndiye mchezaji pekee kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara aliyeweza kupenya kwenye orodha hiyo, akichuana na wachezaji wengine wanaotoka katika ligi za Afrika kaskazini

Kapombe atachuana na mastaa kama Fiston Kalala Mayele wa Pyramids FC, Ismail Belkacemi wa Al Ahli (Libya), Ibrahim Blati Touré wa Pyramids, Issoufou Dayo (zamani wa RS Berkane), na Emam Ashour wa Al Ahly ,Ibrahim Adel (aliyehamia Al Jazeera FC ya Saudi Arabia), Mohamed Hrimat wa AS FAR Rabat, Mohamed Chibi wa Pyramids na Oussama Lamlioui wa RS Berkane.

Uteuzi huu wa Simba SC na Kapombe unaonyesha jinsi soka la Tanzania linavyozidi kupiga hatua barani Afrika, likionesha ushindani na ubora unaoweza kushindana na vilabu vikubwa kutoka Afrika Kaskazini na Kusini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments