SERIKALI YA ZAMBIA YAISUSIA TIMU YA TAIFA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Serikali nchini Zambia imetamgaza kuusitisha msaada wa kifedha kwa timu hiyo baada ya kufanya vibaya kuelekea kufuzu kombe la Dunia 2026, uamuzi huo unakuja baada ya timu hiyo kukubali kipigo Cha 1-0 dhidi ya Niger wakiwa nyumbani.

Kupitia barua iliyotumwa kwenye shirikisho la mpira nchini humo (FAZ) wizara ya michezo inahitaji kujua sababu na maelezo kuhusu ufundishwashi wa timu hiyo na majibu yanatakiwa yatolewe ndani wiki Moja.

Serikali imesema kuwa inatumia gharama kubwa ikiwemo kulipa mishahara, bonasi, usafiri na malazi hivyo serikali inahitaji ufafanuzi ni kwanini waendelee kutoa fedha kwa timu hiyo ilihali inapata matokeo mabovu.


Majibu yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku yenye maelezo kuhusu sakata Hilo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments