Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Uongozi wa Klabu ya Costal Union umethinitisha kusitisha mkataba na kocha mkuu Ali Mohammed Ameir kwa makubaliano ya pande zote mbili, ambapo klabu imemshukuru kocha huyo kwa kuwaongoza kwa kipindi chote alichokuwepi klabuni hapo.
Ameir, katika michezo mitatu ya ligi aliyocheza amepata ushindi mmoja na kupoteza michezo miwili hata hivyo klabu ipo katika hatua za mwisho za kumtambulisha Mohamed Muya kuchukua nafasi ya Ameir klabuni hapo.
Ni michezo michache imepigwa katika ligi ya NBC lakini presha kubwa inawaangukia makocha katika mechezo ya awali kabisa tayali klabu ya Simba imesha achana na kocha wake, Pia mashabiki wa Yanga Wanashinikiza kuondoka kwa Folz , huku Costal Union wakiachana na kocha wao.
Swali ni je, timu za Tanzania hazina uvumilivu kusubiri walau katikati ya msimu?, maana imekuwa mapema sana timu bado hazijapata Ile radha kamili ya ligi, bado wachezaji hawajapata muunganiko kamili lakini kufanya vibaya kwa mchezo mmoja au miwili kunamfanya kocha aachishwe kazi?, timu zetu zinapaswa kujitafakari na kuwapa muda waalimu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment