PSG WAMOTO SAFARI YA KUTETEA TAJI UEFA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya PSG ya nchini ufaransa imeendeleza ubabe wake katika mashindano ya Uefa Champion league baada ya hapo Jana kuibuka na ushindi wa 2-1wakiwa ugenini dhidi ya FC Barcelona.

Mchezo huo ulisubiriwa na mashabiki wa soka ulimwenguni baada ya msimu uliomalizika timu hizo kushindwa kukutana baada ya Barcelona kuondoshwa hatua ya nusu fainali na Inter Milan, mchezo huu ulisubiriwa kwa hamu kutokana na ubora wa uchezaji kwa timu zote ambapo zimekuwa zikicheza aina Moja ya mpira ambayo ni kumiliki mpira huku wakishindwa kwa ushawishi.

Kutokana na aina Yao ya uchezaji matamanio kwa mashabiki yalikuwa ni kuona iwapo timu hizi zikikutana matokeo yatakuwaje na hapo Jana utepe umekatwa kwa PSG kuwachapa Barcelona kwenye ardhi ya ugenini, ambapo Barcelona walikuwa wakwanza kupata kupitia kwa Ferran Torres 19' huku mabao ya PSG yaliwekwa kimiani na Senny Mayulu 38' na Goncalo Ramos 90' na kuhitimisha ushindi huo.

Unaweza kusema PSG ilipata ushindi kwa bahati lakini sio kweli ushindi huo walistahili kutokana na takwimu hizi.



PSG waliumiliki mchezo kwa asilimia 53 dhidi ya 43 ya wapinzani wao huku walipiga Jumla ya mashuti 15 yaliyo lenga lango yakiwa Saba nakuzalisha mabao mawili, huku Barcelona walipiga Jumla ya mashuti 12 huku mashuti yaliyo lenga lango yakiwa matatu yaliyo zalisha bao Moja, kwa twakwimu hizo zinaonyesha PSG aliwazidi wapinzani wake Kila eneo licha ya kuwa ugenini.

Matokeo haya yameibua hisia mseto kuhusu PSG kutete ubingwa mara baada ya kushinda michezo mkubwa hapo Jana , ikumbukwe kabla ya mchezo huo waliichapa Atalanta bao 4-0 na ushindi wa Jana unawafanya wakifikishe alama sita wakiwa wameshindwa michezo Yao yote kinacho subiriwa ni michezo inayofuata kuona kama timu hiyo itaendelea na ubora wake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

 

0/Post a Comment/Comments