PANTEV ANUKIA MSIMBAZI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Katika hatua ya haraka ya kuziba pengo la kocha mkuu ndani ya klabu ya Simba  taarifa zinaeleza tayali wamemalizana na kocha wa kimataifa kutoka Bulgaria, Dimitar Pantev (49), aliyekuwa akiinoa Gaborone United ya Botswana.

Pantev, ambaye ameaga rasmi kikosi cha Gaborone United, anatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam muda wowote  ili kujiunga na miamba na kuanza kazi yake rasmi Msimbazi, Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba tayari umekubali masharti yote aliyoyaweka kocha huyo, ikiwemo mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu ya kuimarisha timu hiyo.



Ujio wa kocha huyu unakuja katika kipindi ambacho Simba inahitaji kurejesha makali yake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, hususani kwenye michuano ya kimataifa, Wataalamu wa soka wanasema Pantev ni kocha mwenye mbinu za kisasa, anayeamini katika soka la kushambulia kwa nidhamu ya kiufundi, jambo ambalo linaweza kuipa Simba sura mpya baada ya misimu michache ya sintofahamu ya makocha kutokaa muda mrefu.

Kwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi, matumaini mapya sasa yamezaliwa ,Wanaamini mikoba ya Fadlu Davids aliyewapeleka hatua kubwa inaweza kushikiliwa na kuendelezwa vyema na kocha huyu mpya kutoka Bulgaria.



Macho yote sasa yameelekezwa Dar es Salaam, kusubiri ujio wa Dimitar Pantev na mwanzo mpya wa safari ya Simba SC.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

 

0/Post a Comment/Comments