Mwanakwetusports.
Ligi kuu Tanzania Bara (NBC), imegeuka moto unatumika kung'arishia dhahabu kutokana na kutambulisha vipaji vikubwa vilivyo jificha gizani kimataifa na hii inachagizwa na ubora wa ligi hiyo yakiwa ni matunda ya uwekezaji na uongozi imara.
Nyota wa klabu ya Yanga Africa Pacome zouzoua nikipaji ambacho kilijificha gizani lakini wananchi walikiona na kukileta nchini, akiwa klabuni hapo ameonyesha uwezo wa Hali ya juu ikiwemo kufanya maamuzi katika michezo mkubwa kwenye ligi ya ndani pia kimataifa.
Kutokana na kipaji chake kuonekana timu ya Taifa ya Ivory coast ikamjuisha marakadhaa kwenye timu hiyo na kuonyesha kuwa ni mchezaji mkomavu .kwenye mchezo wao wa kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Seychelles alicheza dakika zote tisini katika ushindi wa 7-0 wakiwa ugenini.
Hiyo inamaanisha kuwa ligi yetu inakuwa na inatazamwa kwa hicho la tatu kama sehemu ya kuwanoa mastaa, ikumbukwe kipindi Cha nyuma ilikuwa ni ngumu kwa ligi yetu kutoa wachezaji kucheza timu za Afrika magharibi na kumbukwe Senegal walisha mjumuisha Pape Sako kutokea Simba katika kikosi Chao wapo Wengi ila Sako na Pacome ni mfano halisi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment