OLMO KWENYE MEZA YA MATIBABU, HATI HATI KUIKOSA EL CLASICO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports,

Klabu ya FC Barcelona imethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Dani Olmo amekumbwa na jeraha la msuli kwenye miguu wake wa kushoto kitu ambacho kinamuweka nje ya uwanja kwa wiki mbili hadi tatu.

Olmo anaungana na Lamine Yamal pamoja na Ferran Torres kwenye orodha ya majeruhi klabuni hapo, sasa mchezaji huyo anauguza jeraha lake baada ya kurejeshwa nyumbani kutoka timu ya Taifa wiki iliyopita.

Hivyo, Olmo yupo kwenye hati hati za kuukosa mchezo wa El clasico dhidi ya wapinzani wao wakubwa klabu ya Real Madrid mchezo unaotarajiwa kupigwa siku ya Oktoba 26, 2025 katika dimba la Santiago Bernabeu.

Msululu wa majeraha umeanza kuindama klabu ya Barcelona kwa wachezaji wao muhimu kuumia wakati ambapo timu imekuwa ikiwahitaji na hii inasababishwa na wachezaji kucheza michezo mfululizo bila kupata mapumziko kitu ambacho kinaweza igharimu timu kwa kupata matokeo mabovu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments