Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Beki kisiki wa klabu ya Simba Rushine De reuck amezidi kutakata katika ligi kuu Bara baada ya hapo Jana kuifungia timu yake bao dakika ya 63' kwenye ushindi wa 3-0 walioupata dhidi ya Namungo kwenye dimba la Benjamin mkapa huku akiibuka nyota wa mchezo.
Rushine, anafikisha bao lake la pili katika michezo miwili ya ligi akiwapiku washambuliaji wa timu hiyo ambapo baada michezo hiyo yeye ndiye kinara wa upachikaji mabao klabuni hapo, beki huyo anaonekana yuko bora katika eneo zaidi ya Moja kuanzia ulinzi , kuanzisha mashambulizi hadi ufungaji vitu ambavyo wananvyo mabeki wachache sana Duniani.
Sifa kubwa ya Rushine ni utulivu, nidhamu na ufanisi akiwa uwanji kitu kinachomfanya kutekeleza majukumu yake kwa usahihi licha ya kufunga mabao hayo pia hajaruhusu ngome yake kutikiswa mpaka sasa.
Huenda mjadala wa tuzo ya beki bora ukazimwa mapema kama kitasa hiki kikizidi kuonyesha kiwango hiki hiki, lakini bado ni mapema kusema hivyo ila dalili na uwezo wa mchezaji unainekana na huenda huyu akawa ni X-factor pale msimbazi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com
Post a Comment